Miradi saba ya maji kuibadilisha Ludewa

NJOMBE: MKUU wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva amefanya ziara ya kimkakati ya ukaguzi wa miradi ya maji wilayani Ludewa.

Akitembelea miradi mbalimbali Victoria amesema lengo ni kuhakikisha kuwa wana-Ludewa wanapata huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza sambamba na kuonesha kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya maji Ludewa.

Aidha, katika ziara hiyo imethibitika kuwa Wilaya ya Ludewa inaendelea kutekeleza miradi saba ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 13.

Victoria amesema kukamilika kwa miradi hiyo kunalenga kuongeza huduma ya maji kutoka asimia 74.

3 hadi asilimia 79.7 eneo la vijijini na asimia 100 kwa wakazi wa Mji wa Ludewa.

Pia amepokea taarifa za miradi wilaya nzima na kutembelea miradi iliyopo Kata za- Mavanga, Ludewa, Iwela, na Manda katika kukagua hali ya upatikanaji wa maji na hali za miradi.

Aidha, ametembelea vyanzo vya maji vya Mavanga na kumkagua mkandarasi anayelaza mabomba eneo la Nyamapinda, na kutembelea ujenzi wa ofisi ya vyombo vya usimamizi wa watumia maji ngazi ya jamii CBWSO- na kukagua vituo vya ugawaji wa maji kwenye jamii. Pia amekagua zoezi la uchimbaji visima linaloendelea Kata ya Manda.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button