Miradi ya bil 5/- ina upungufu Tanga

TANGA: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Tanga imebaini upungufu katika miradi ya maendeleo 12 ya maji, afya na elimu yenye thamani ya Sh bilioni 5.4.
Akitoa taarifa ya utendajikazi wa taasisi hiyo katika kipindi Januari hadi Machi mwaka huu leo Mei 30, 2025, Naibu Mkuu wa Taasisi hiyo mkoani hapa, Marium Mayaya amesema baada ya uchunguzi walibaini miradi hiyo haijakidhi ubora wa thamani halisi ya fedha.
SOMA ZAIDI
Amesema kuwa katika ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma walikagua jumla ya miradi 54 ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 240.2 na kubaini miradi 12 yenye mapungufu.
“Tuliweza kubaini miradi hiyo ipo katika hali isiyokidhi ubora kulingana na thamani ya fedha zilizowekezwa na hivyo kutoa ushauri wa marekebisho ya upungufu hayo,” amesema Mayaya.



