“Miradi ya ujenzi itoe ajira kwa wananchi”

SOMA ZAIDI:
Akizungumza na wafanyakazi wa mradi huo Ulega amesema: “Barabara hii si ya mchina, ni yetu watanzania, msifanye udokozi, fanyeni kazi kwa kujituma ili mradi unapoisha muwe mmepata maarifa ambayo yatakusaidia kuwa fundi mzuri”.
Waziri Ulega ameeleza kuwa serikali imeanza mchakato wa kuwarasimisha mafundi wasio rasmi ambao hawajapita kwenye vyuo vya mafunzo ya ufundi ila wana uzoefu wa ujenzi ili wapewe ajira hivyo kuzitaka mamlaka pamoja na wakandarasi kutoa vyeti kwa wafundi pindi mradi unapokamilika vitakavyowawezesha kutambuliwa.
Aidha, Waziri Ulega amemtaka mkandarasi huyo kufanya kazi kwa wakati na kwa ubora kwani tayari Serikali imeshamlipa malipo ya awali.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amemshukuru Waziri Ulega pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua Mtwara kwa miradi mbalimbali ya maendeleo.



