Miriam Odemba kuiteka Dar, tukio la mitindo

DAR ES SALAAM: MWANAMITINDO raia wa Tanzania, Miriam Odemba anayeishi Ufaransa na Hispania, Miriam Odemba amesema ameanda tukio kubwa kwa ajili ya wadau wa mitindo.
Miriam ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Miriam Odemba Foundation ( MOF ) amesema atafanya tukio hilo Agosti 9, 2025 mara baada ya kurejea nchini kutoka nje.
Aidha, ameeleza lengo la tukio hilo ni kutathmimi ubunifu wa Kitanzania, kupata madini kutoka kwa wabunifu mashuhuri na utoaji wa zawadi muhimu alizoandaa.
” Hii sihitaji mpaka siku ya tukio ni bonge moja la ‘suprise’ uzuri ni kwamba kila mmoja anaweza kushiriki,” ameeleza Miriam.