Miriam Odemba: Mafanikio sio hadhi bali bidii, utu, nidhamu

DAR ES SALAAM: MWANAMITINDO maarufu nchini, Miriam Odemba amesema mafanikio pekee hayategemei hadhi, wadhifa au asili ya mtu, bali bidii, nidhamu, nia na dhamira ya kuinua wengine.

Akizungumzia historia yake yenye lengo la kuinua wengine, Miriam amesema anajivunia kupata maneno ya pongezi na moyo wa upendo kutoka kwa wafuatiliaji wa safari ya maisha yake.

Miriam ameiambia HabariLEO kuwa: “Kufahamika na kujulikana katika mambo mbalimbali ikiwemo mitindo na urembo nakuheshimika na jamii nzima kwenye maadili, utu usawa na kujali”.

Miongoni mwa watu maarufu ambao wametoa pongezi hizo ni mdau maarufu wa muziki nchini Madam Rita, na wengine wengi.


Baada ya kupokea pongezi hizo, Miriam amesema licha ya kazi kubwa na umaarufu wake ila wapo wanaodhani anastahili kuwa kiongozi mwenye madaraka katika jamii, na wengine kusisitiza kuendelea kukiasa kizazi kinachokuja ila wanapaswa kutambua kuwa yeye ni mama anayesimama katika nafasi yake na kusaidia jamii na sio kama mtu maarufu.


“Kwa moyo wa shukrani na kusudi njema ninaendelea kuwajibika na ninamhamasisha kila mwanamke, binti, mama, na hata kiongozi wa ngazi yoyote ile kusimama katika nafasi yako na kuisaidia jamii yako kwa kadri unavyoweza,” ameongeza Miriam.

Miriam amesema mtu yoyote katika jamii au nafasi yake anaweza kufikia ndoto zake katika mitindo au urembo bila kujali ukubwa wa mtu.

“Nimepata nafasi katika urembo na mitindo, na wewe pia unaweza katika nafasi yako, haijalishi ukubwa, hata ukiwa mama ntilie wa mtaani, una nafasi ya kuisaidia jamii yako inayokuzunguka,” amesema Miriam.

Hata hivyo Miriam amesema anakubali kuendelea na safari yake na kuwa sehemu ya mabadiliko ikiwemo kusimama na kupaza sauti na kulea wale wenye ndoto kubwa katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Habari Zifananazo

6 Comments

  1. Hello to every body, it’s myy first pay a vvisit of this blog; his website ccarries amazimg
    andd really fine information in support off visitors.

  2. It’s actuzlly a great andd uszeful piewce of info.
    I am happy thqt youu simply shared this useful nformation wifh us.
    Pleasze stay uus informed like this. Thajks ffor sharing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button