Misitu ikitazamwa upya itaongeza zaidi pato la taifa

RASILIMALI misitu, kwa kiasi kikubwa huhifadhi mazingira na kuimarisha hali ya hewa inayochangia uzalishaji mali kwenye sekta nyingine za uchumi mfano, kilimo na usalama wa chakula, nishati, mifugo, uvuvi, wanyamapori, maji, utalii, afya na elimu.
Hata hivyo, huduma za kiikolojia zitokanazo na rasilimali misitu, kwa miongo kadhaa zimekuwa hazithaminiwi (kifedha) kwenye uchumi na kitaifa.
Uzoefu unaonesha kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imekuwa ikitoa taarifa kila mwaka kuhusu mchango wa rasilimali misitu kwenye pato la taifa lakini kwa kutumia asilimia ndogo. Kwa bahati mbaya, huduma za mifumo ya ikolojia ya sekta ya misitu, ambayo haiko kibiashara imekuwa haijumuishwi kama sehemu ya mchango wa misitu katika Pato la Jumla la Taifa (GDP).
Aidha, kwa miaka mingi rasilimali misitu imekuwa hazina muhimu inayotegemewa kama chanzo cha kuwezesha wananchi kuyamudu maisha vijijini na mjini.
Hivyo, mfumo wa NBS kuweka bayana mchango wa sekta mbalimbali kwenye GDP, umekuwa ukizingatia zaidi mapato ya misitu kutokana na mazao yaliyouzwa. Utaratibu husika umekuwa hautilii maanani huduma ya ikolojia ya misitu.
SOMA: TFS, wadau mazao ya misitu wateta
Kwa miaka kadhaa, wataalamu wa misitu wamekuwa wakieleza kukosekana uthamanishaji wa ikolojia ya misitu, ili thamani yake iwe sehemu ya mchango wa sekta ya misitu kwenye GDP. Hata hivyo, sauti husika zimekuwa hazipenyi kutokana na kutofautiana kimtazamo kitaaluma na kisiasa.
Hoja kuu kuhusu michakato ya huduma za ikolojia ambazo haziko rasimu kibiashara inahusisha masuala kama vile misitu na virutubisha udongo, kuhifadhi vyanzo vya maji, kudumisha bayoanuwai, hifadhi ya kaboni na mengineyo.
Mathalani, katika mazingira yenye misitu asilia inakuwa rahisi kudhibiti mvua na kuwezesha maji yasipotee na wakati huo huo misitu ikirutubisha udongo na kuhifadhi viumbe hai, sambamba na kutunza makazi ya wanyamapori na kupunguza kaboni angani, hivyo kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kadhalika, bayoanuwai zilizomo kwenye msitu kama nyuki huweza kufanya uchavushaji ipasavyo na kuimarisha uzalishaji mazao shambani wakati wanapotafuta nekta kwa ajili ya kutengeneza asali.
Kwa mujibu wa NBS mwaka 2023, mchango wa sekta ya misitu katika GDP, kati ya mwaka 2010 na 2023 ulikadiriwa kuwa kati ya asilimia 2.2 na asilimia 4.
Mwaka 2019 hadi 2021, serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ilifanya utafiti kuhusu mchango wa misitu kwenye uchumi bila kuhusisha huduma za ikolojia ya misitu na kuripoti mchango wa asilimia 3.3 katika GDP. Kwa hiyo, ripoti za NBS na wizara zilithaminisha mchango wa misitu kwa kutumia viashiria vya kawaida vya kiuchumi kama vile ajira na mapato yanayotokana na bidhaa za misitu zilizouzwa.
Kwa kuwa mbinu za kawaida hazizingatii huduma za mifumo ya ikolojia katika hesabu za GDP, iliilazimu serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya utafiti zaidi ili kubaini uhalali wa huduma za ikolojia katika kuthaminisha mchango halisi wa misitu kwenye GDP.
Kutokana na umuhimu wa suala hilo Wizara ya Maliasili na Utalii iliwezesha Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kufanya utafiti ili kubainisha mchango wa huduma za ikolojia zitokanazo na uwepo wa misitu asilia maeneo mbalimbali nchini.
Utafiti huo ulihusisha wajumbe kumi; watatu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), wawili kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM), wawili kutoka TAFORI na watatu wengine kutoka Idara ya Misitu na Nyuki, NBC na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Pia, utafiti huo ulilenga uthaminishaji wa huduma za ikolojia na kupata thamani yake kifedha, ili kupata msingi wa uhakika wa kitaaluma wa kuwashawishi watumiaji wa rasilimali misitu na vyombo vya maamuzi watambue kikamilifu thamani yake na hatimaye waweze kufanya maamuzi yenye uelewa wa kutosha na mtazamo chanya, waweze kutoa kipaumbele kudumisha uhifadhi misitu asilia kwa manufaa ya wengi.
Inatia moyo kwamba, kupitia utafiti uliofanyika umeweza kuthibitisha thamani yake hivyo kubainisha huduma ya ikolojia ya misitu inaweza kuchangia asilimia 16.73 kwenye GDP. Hakika huo ni mchango mkubwa ambao hauonekani kifedha lakini ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi.
Haya ni matokeo ya mbinu za uthaminishaji kijani, utaratibu ambao haujawahi kutumiwa nchini ingawa umekuwa ukitumiwa na nchi nyingine kama China. Takwimu hizo zikijumuishwa na asilimia 3.3 kama mchango wa misitu wa sasa kwenye GDP inafanya mchango halisi wa misitu kufikia asilimia 20.03 hivyo, kuweka bayana thamani na umuhimu wa rasilimali misitu nchini.
Matokeo kuhusu thamani ya ikolojia misitu kwa kutumia uthamanishaji kijani yanapaswa kuwawezesha watunga sera na wafanya maamuzi kutafakari kwa kina kuhusu huduma ikolojia misitu, ili kuimarisha uendelevu wa rasilimali misitu nchini.
Kutokana na matokeo haya na kufikia mwafaka kitaifa, inashauriwa serikali na wadau wote, kukomesha mara moja shughuli zinazosababisha huduma ya ikolojia misitu kuzorota ikiwemo ukataji miti, uharibifu wa misitu kupitia kilimo na ukataji na uchomaji hovyo wa misitu.
Yote hayo na mengine yanayofanana nayo yanapaswa kudhibitiwa ipasavyo. Kulingana na takwimu zilizopo, kiwango cha upotevu wa rasilimali za misitu ni takribani hekta 470,000 kila mwaka, jambo ambalo linatishia huduma za ikolojia ya misitu.
Thamani ya ikolojia kupitia rasilimali za misitu katika GDP, inathibitisha umuhimu wa kuhifadhi misitu asilia kuliko kuibadilisha kwa matumizi mengine. Wizara husika inapaswa kubuni mifumo inayoweza kutumika kuwezesha walengwa wote kuchangia katika uhifadhi wa misitu.
Mfano, kuanzisha malipo ya Huduma za Mfumo wa Ikolojia (PES) kwa kuzingatia faida za kiuchumi na mitazamo chanya, ikiwemo utashi wa kisiasa.
Pamoja na hayo, Wizara inapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha NBS, kila mwaka inapata takwimu sahihi kuhusu mchango wa misitu kenye uchumi wa nchi kwa kujumuisha mchango wa huduma ya ikolojia ya misitu kupitia takwimu za uthaminishaji kijani na nyinginezo.
Kwa sasa thamani iliyotokana na utafiti huu ichukuliwe kwa uzito wake kama msingi wa kuanzia.
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Cash earning job to earns more than $300 per day. getting paid weekly more than $2300 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
.
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com