Misri yaivua ubingwa Ivory Coast

MOROCCO; MISRI imefuzu nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2025, baada ya usiku huu kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya bingwa mtetezi Ivory Coast.
Mabao ya washindi yamefungwa na Omar Marmoush (dakika ya nne), Ramy Rabia (32) na Mohamed Sakah (52), wakati ya Ivory Coast yamefungwa na Ahmed Abou El Fotouh ambaye alijifunga dakika ya 40 na Guela Doue (73).



