DAR-ES-SALAAM : UTAMADUNI wa Kisomali unamuongoza mwanamke wa Kisomali kama mtu wa kipekee ambaye jukumu lake ni uangalizi wa familia na uzalishaji, nikimaanisha usimamizi wa mifugo na kuongeza familia.
Mfumo dume umetawala karne na karne katika familia za Kisomali, ambapo mwanamke hana uwezo wa kufanya kitu sawa na mwanaume, huku wakifuata zaidi na miongozi ya kidini.
Hapo mwanzo walikuwa wanatumiwa kama vyanzo vya mtaji kwa jamii inayowazunguka, lakini ndoa zao zilianza kubadilika baada ya wanawake hawa wa kisomali kuolewa na jamii zingine tofauti.
Ingawa tamaduni za kibaba zilikuwa zinatawala na kutambua majukumu yao hasa kama wake na mama, wanawake wa Kisomali walitumia tamaduni hizo pamoja na rasilimali za kienyeji zilizokuwapo kuweza kufanya maamuzi, kujadiliana nafasi zao, na kuunda maeneo yao binafsi.
Kuletwa kwa utawala wa kikoloni, kuligawanya wasomali kati ya Uingereza, Ufaransa, Italia, na himaya ya Ethiopia, kulileta mabadiliko makubwa katika maisha ya wanawake.
Kulileta muunganiko wa uhusiano wa kibaba na uhusiano wa Kiebrania, kuandika sheria za jadi na kutambulika kwa majukumu ya jamii, na kuwafanya wanawake kama wategemezi wa jamaa zao za kiume, huku likiunda fursa za kimasomo na ajira kwa wanaume, ambazo hazikuwapo kwa wanawake.
Ingawa wanawake wa Kisomali walikuwa mstari wa mbele katika harakati za kupinga ukoloni, kundi la wanaume wa tabaka la juu waliorithi utawala baada ya uhuru walizuwia wanawake kuingia kwenye siasa.
Haki za wanawake zilichukua nafasi muhimu katika utawala wa kijeshi wa Jenerali Mohamed Siad Barre, lakini ukandamizaji na ukatili wa kifedha ulioambatana na utawala wake ulishuhudia athari kubwa kwa wanawake.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyofuatia baada ya kuvunjika kwa serikali ya Kisomali vimeathiri wanawake kwa karibu.
Mbali na uzoefu wa ukatili wa kijinsia, hali ya kihafidhina ya jamii ya Kisomali imefanya kupotea kwa mafanikio mengi yaliyopatikana kwa haki za wanawake baada ya uhuru.
Kutoka kwa jamii ya kabla ya ukoloni, utawala wa kikoloni, utawala wa kijeshi, na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wanawake wa Kisomali wameonesha uthubutu wa uwezo wao wa kufanya maamuzi , na nguvu ya kuleta mabadiliko hata katika hali ngumu za maisha.
Khadija Omar ni msichana mwenye umri wa miaka 23, ambaye ameonesha mfano kwa jamii ya Kisomali na jamii ya Kiislamu katika mashindano ya dunia ya ulimbwende Miss Universe 2024, amekabidhiwa taji la Miss Universe 2024 katika ukanda wa Afrika.
Ushiriki wake umetengeneza historia kubwa na ya kipekee kama mwanamke wa kwanza kuvaa hijabu kuwakilisha nchi yake katika mashindano ya Miss Universe yenye heshima kubwa duniani.
Mrembo huyu alizaliwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Hagadera nchini Kenya, na safari ya Khadija kutoka mkimbizi hadi kuwa mshiriki wa mashindano ya urembo ya kimataifa ni ya kipekee.
Yeye pia ni Miss Universe Somalia wa kwanza kushiriki katika kiwango hiki, akianzisha hatua mpya kwa taifa la Somalia. SOMA : Miss Universe Afrika Kusini avuliwa uraia
Mnamo mwaka 2010, Mrembo Khadija na familia yake walihamia nchini Kanada, ambapo alipata mabadiliko makubwa ambayo yalichangia katika kuunda mwelekeo mpya wa maisha yake.
Kukulia katika nchi mpya kulimwezesha kukumbatia mizizi yake ya Kisomali, huku akikutana na fursa na changamoto za mazingira tofauti ya mila na desturi.
Uzoefu wake wa mitindo na urembo ulimfanya Khadija kuwa na shauku kubwa ya kuwakilisha wanawake wa Kisomali na wanawake Waislamu duniani kote, ambapo viwango vya uzuri na utofauti bado vinabadilika.
Ushiriki wa Khadija katika Miss Universe unawakilisha zaidi ya uzuri; unasimamia ustahamilivu wa wanawake wa Kisomali na jamii kubwa ya Waislamu.
Wakati katika amshindano haya mrembo Khadija alishiriki akiwa amevaa hijabu, Khadija anataka kupinga dhana potofu na kubadilisha mifumo …