Mkakati wasukwa huduma za afya, upunguzaji gharama

DAR ES SALAAM: TANZANIA imeanza mchakato wa kuboresha huduma za afya shirikishi na ufadhili endelevu ili kuongeza ufanisi, kupunguza gharama na kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa Watanzania.
Hatua hiyo inalenga kuboresha mfumo wa utoaji huduma za afya shirikishi kwa lengo la kuongeza ufanisi, kupanua upatikanaji wa huduma bora, na kuhakikisha mfumo endelevu wa ufadhili wa sekta ya afya.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), George Ruhago amesema maboresho yanalenga kuunganisha huduma kama vile VVU na UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) kama vile shinikizo la damu na kisukari, ili wagonjwa waweze kupata huduma kamili kwa ziara moja kituoni.
Ruhago amesema wamepata nafasi ya kupitia na kuboresha mfumo wa utambuzi na upangaji gharama za utoaji wa huduma shirikishi kwa magonjwa hayo kwa kutumia mbinu bunifu za kisayansi zitakazowezesha huduma bora zaidi kwa gharama nafuu.
“Ukimwi na magonjwa yasiyoambukiza ndio unaochukuwa gharama kubwa katika utoaji wa huduma, kwa hiyo tulikuwa tunajaribu kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuhuisha hizi huduma zikatolewa kwa wengi kwa gharama nafuu,”
“Kwa hiyo moja wapo ilikuwa kutafuta mfumo, tunajaribu kuangalia gharama za utoaji huduma, mifumo, muda na maeneo gani ambayo sasa huduma kwa mfano magonjwa yasiyoambukiza yanaweza kuungana zikatoa huduma,” amesema Ruhago.
Mtaalamu wa magonjwa ya kisukari, Kaushik Ramaiya amesema sababu ya kuanza utafiti na majadiliano hayo ni baada ya kuona wagonjwa wa ukimwi wanalazimika kwenda kwenye kliniki nyingine baada ya kugundulika wana ugonjwa mwingine tofauti na ule uliompeleka hospitali.
“Unakuta mgonjwa anakuja katika kliniki ya ukimwi anaambiwa mambo ya presha nenda kwenye kliniki nyingine, hivyo tunaona kama tunaweza kuunganishi hizi huduma ziwe ‘one stop clinic’ itatusaidia wananchi wasipate shida.
Daktari na Mchumi kutoka MUHAS, Dk Frida Ngalesoni, ameeleza kuwa eneo lingine lililoangaziwa ni kuhusu ugonjwa wa sikoseli ambapo eneo ambalo watoto wanapatiwa chanjo liwe na uwezo pia kuwapima ugonjwa huo mapema na kuwapa tiba.
“Tusipofanya hivyo tutakuwa kama tunaongeza gharama nyingi kwenda kutibu ugonjwa ambao umeleta shida nyingi tukichelewa kuukamata mapema, badala ya kumwambia njoo kliniki nyingine unamshika palepale,” amesema Dk Frida.
Warsha hiyo imekutanisha wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), vyuo vikuu vya Harvard na Boston (Marekani), ambapo wamekutana jijini Dar es Salaam na wataalamu kutoka Wizara ya Afya, TAMISEMI, TACAIDS, NASHCoP, pamoja na wadau wa maendeleo akiwemo Ubalozi wa Marekani (Office of Foreign Assistance), FCDO kutoka ubalozi wa Uingereza, EGPAF, CHAI, Chama cha Kisukari Tanzania Diabetics Association of Tanzania (TDA), NIMR, Hospitali ya Amana na Jiji la Dar es Salaam.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com