Mkalama wataka mafuta ya kupikia yawekewe kodi

Wananchi wa Mkalama wameiomba serikali kuweka kodi kwenye mafuta ya kupikia yanayotoka nje ili kunusuru zao la alizeti ambalo sasa bei yake imeshuka.

Akizungumza katika ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo leo wilayani hapa,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba amesema bei ya alizeti imeshuka kutokana na mafuta ya kupikia kutoka nje kuingia nchini bila kodi.

“Serikali ilituhamasisha tuhamasishe wakulima kulima kwa wingi alizeti na ikatuoa mbegu bora,tumelima bei ni ndogo hairudishi hata gharama za mkulima,”amesema Serukamba.

Hivyo akaomba serikali iweke kodi kwa mafuta hayo kutoka nje ili alizeti ipate soko na kuwakwamua wananchi na umaskini.

Habari Zifananazo

Back to top button