Mkurugenzi Puma ashauri wakuu taasisi za umma kuepuka urasimu

Puma Energy Tanzania yashauri SOEs kuboresha utendaji na huduma

ARUSHA: Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah amewashauri wakuu wa taasisi zilizo chini ya Serikali kuzingatia ubunifu na kuondokana na urasimu ikiwa ni moja ya njia ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

Mkuu wa Puma Tanzania alitoa rai hiyo jijini Arusha hivi karibuni wakati akiwasilisha mada katika mkutano uliowaleta pamoja wenyeviti wa bodi na wakurugenzi wakuu wa taasisi za umma.

Katika wasilisho lake, Fatma alishauri kuachana na urasimu na kuzingatia mbinu bunifu za kisasa ambazo zitarahisisha taratibu za kiutendaji na kuharakisha utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi.

SOMA: Puma Energy yampongeza Rais Samia mazingira bora ya uwekezaji nchini

Alisisitiza pia umuhimu wa kuanzisha mfumo thabiti unaojengwa juu ya utawala bora, uwazi, matumizi sahihi ya data, biashara endelevu na viashiria vya utendaji (KPIs) ili kuongeza tija na kuboresha matokeo ya huduma.

Kwa upande wake, Puma Energy Tanzania inajivunia mafanikio chanya yaliyopatikana kupitia mfumo wa nguzo tano unaojikita kwenye: Uongozi thabiti, Mageuzi ya sera, Miundombinu ya kidijitali, Nguvu kazi yenye wepesi na Utamaduni wa utendaji unaoendeshwa na matokeo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button