Puma Energy yampongeza Rais Samia mazingira bora ya uwekezaji nchini

Rais Samia Suluhu Hassan.

KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji nchini, hivyo kuwezesha kulipa kodi kwa serikali na kuchochea maendeleo.

Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah baada ya kampuni hiyo kuibuka kinara kwa kupokea tuzo nne za mlipakodi bora wa mwaka zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Rais Samia alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam. “Mazingira mazuri na wezeshi yaliyowekwa na serikali chini ya uongozi wa Dk Samia Suluhu Hassan ndiyo yametuwezesha wawekezaji kufanya shughuli zetu katika mazingira mazuri, ndiyo maa[1]na sisi Puma Energy Tanzania tumepata tuzo zote.

Advertisement

“Tumekuwa walipakodi wazuri hususani katika sekta ya mafuta na gesi, ndiyo sababu ya kupata tuzo zote hizo. Kwa hiyo tunamshukuru Mungu lakini tunamshukuru Rais Dk Samia kwa kuweka mazingira yaliyo bora kwa wawekezaji kuendelea kufanya vizuri nchini,” alisema. Fatma alisema wanaona zinakopelekwa fedha zinazotokana na kodi zinazolipwa na hatimaye kuchochea maendeleo makubwa yanayoletwa nchini chini ya Rais Samia.

“Tumeona miradi mikubwa iliyozinduliwa mwaka 2024 lakini kuna miradi mingine mingi ambayo bado iko katika mchakato wa kuzinduliwa, kwa hiyo tunapolipa kodi tunajua fedha zetu zinakwenda wapi,” alieleza. Alisema tuzo zote ambazo Puma Energy Tanzania imezipata kutoka TRA zinatokana na uwajibikaji wao katika kulipa kodi kwa wakati na kwamba tuzo hizo ni chachu ya maandalizi ya mwaka ujao wa fedha kufanya vizuri zaidi.

Kupitia hafla hiyo, Puma Energy Tanzania imetunukiwa tuzo ya mlipakodi anayekidhi Puma Energy yampongeza Rais Samia mazingira bora ya uwekezaji nchini magazeti ya Daily News na HabariLEO yatachapisha kuadhimisha miaka 4 ya mafanikio ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa madarakani. kwa ajili ya kutangaza Matangazo, Makala na Muonekano wa Bidhaa/Taasisi/Kampuni yako na upate punguzo la hadi 20%* na nafasi katika Majukwaa ya Kidijitali ya TSN.

Toleo Maalumu Wahi Nafasi Mapema! Tarehe 19 Machi 2025 Habarileo_tz dailynews_tz spotileo Daily News HabariLeo HabariLeo dailynewstz Daily News Digital Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia: Simu: +255 22 211 6074/0685 425462 au Baruapepe: matangazo@tsn.go.tz *Vigezo na Masharti Kuzingatiwa* ORD8672884 viwango vya ubora katika ngazi ya kitaifa kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Pia, kampuni hiyo kupitia kitengo chake cha Wet Cargo, imepata tuzo ya kutambua malipo ya wakati ya kampuni hiyo ya kodi na ushuru katika mwaka wa fedha 2023/2024 katika forodha na ushuru wakati wa siku ya mlipakodi nchini mwaka 2024.

Tuzo nyingine iliyopata Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited ni ya mshindi wa jumla katika kutambua ulipaji wa kodi na ushuru zilizolipwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 katika forodha na ushuru wakati wa siku ya kuthamini walipakodi mwaka 2024.

Tuzo ya nne imetolewa kwa kampuni hiyo kupitia kitengo cha uagizaji wa Wet Cargo kutambua ushuru mkubwa wa kampuni ulio[1]lipwa katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 katika forodha na ushuru 2024.

Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka hutolewa kila mwaka na TRA ambapo taasisi hiyo hutoa zawadi kwa wafanyabiashara wanaolipa kodi katika makundi mbalimbali.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *