Ulaya yajipanga kuongeza vikwazo

BERLIN : KANSELA wa Ujerumani, Friedrich Merz, amemtuhumu Rais Vladmir Putin kwa kuchelewesha makusudi mazungumzo ya amani na Ukraine.
Akizungumza mjini Berlin baada ya mkutano na Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney, Merz amesema kuwa walitarajia kuona mkutano kati ya Putin na Rais Volodymyr Zelensky ungemalizika ndani ya wiki mbili baada ya kikao cha Alaska, lakini hakuna dalili.
Merz amesema Umoja wa Ulaya unaendelea kujadili vikwazo vipya dhidi ya Urusi kutokana na kushindwa kuonyesha nia ya kumaliza vita Ukraine. SOMA: Marekani yaitaka Urusi kusitisha mapigano