Mkuu wa Mkoa Mtwara ataka jitihada za watendaji kwa wananchi

KATIKA kuelekea mwisho wa mwaka wa 2020/22 Serikali ya Mkoa wa Mtwara imewataka Watendaji Mkoani humo kuendeleza jitihada za kuwatumikia Wananchi ili kila mmoja wao aweze kuridhika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali hiyo katika maeneo yao.

online pharmacy robaxin no prescription with best prices today in the USA

Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abas wakati Uongozi wa Mkoa huo ulipotembelea kwenye eneo la Msanga Mkuu lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara (MSANGA MKUU FESTIVAL 2020/22) ikiwa ni sehemu ya Utalii wa Ufukweni.

Lengo la ziara hiyo ni kujionea mazingira ya eneo hilo la Msanga Mkuu Festival sambamba na kutoa hamasa kwa Wananchi hao ili waweze kijitokeza kwa wingi wakati wanaposherehekea mwaka mpya wa 2020/23.

online pharmacy isofair no prescription with best prices today in the USA

Mkuu huyo wa Mkoa amesema Watumishi hao kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anafanya kazi kwa kasi, ari kubwa kwani kila kitu kipo hivyo hawana sababu ya kulalamika badala yake wawe na jitihada ya kuwahudumia Watu wao

“Huo ndiyo moto wangu, kila mmoja ahakikishe anafanya kazi kwa kasi, ari kubwa kwasababu hatuna sababu ya kulalamika kila kitu kipo ndani ya uwezo wetu tujitahidi kuwahudumia Watu wetu”,amesema Abas

Sanjali na hilo Mkuu huyo wa Mkoa amewatahadharisha Wananchi Mkoani humo hasa Kufuatia kuwepo kwa ongezeko la ajali katika maeneo mbalimbali Nchini, wawe makini na kuzingatia Sheria pindi wanapoendesha vyombo vyao vya moto.

Pia amewahakikishia Wananchi hao suala la ulinzi na usala hasa wanapoelekea kusherehekea mwaka mpya wa 2020/23 kwamba hali ya usalama iko vizuri kwani Vyombo vyote viko imara na makini hivyo waje kwa wingi kwenye eneo hilo la Msanga Mkuu Festival ili waweze kusherehekea mwaka mpya huo wakiwa na uhakika na usalama wao.

Diwani wa Kata ya Msanga Mkuu kwenye Halmashauri hiyo Mariamu Lilepe ameishukuru na kuipongeza Serikali kwa kuwapatia fursa hiyo kubwa kwao hasa Vijana wa maeneo hayo.

online pharmacy mobic no prescription with best prices today in the USA

“Kuja kwa Festival hii kwetu sisi wana Msanga Mkuu ni fursa kubwa sana kwa Vijana wetu na wenyewe Vijana wanasema huu ni muda wa mavuno kwahiyo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa niseme asante sana kwa niaba ya Wananchi wa Msanga Mkuu”,amesema Lilepe

Habari Zifananazo

Back to top button