Mlanguzi wa dawa za kulevya akamatwa

MEXICO: ALIYEKUWA kiongozi wa magendo nchini Mexico, Ismael “El Mayo” Zambada, amekiri kushiriki katika vitendo vya ulanguzi wa dawa za kulevya kuelekea Marekani.

Zambada amesema anajutia kuhusika kwake katika usafirishaji wa kokeini, heroini na dawa nyingine haramu, hatua iliyochochea ghasia mbaya nchini Mexico.

Katika maelezo yake, ameeleza kuwa anabeba dhamana kikamilifu kwa matendo hayo na kuomba radhi kwa madhara yaliyosababishwa na mtandao huo wa uhalifu. SOMA: Tani 18 dawa za kulevya zadakwa Dar

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, chini ya uongozi wa Zambada na Joaquin “El Chapo” Guzmán, kundi la Sinaloa Cartel lilipanuka kutoka mtandao wa kikanda hadi kuwa moja ya mitandao mikubwa zaidi ya biashara ya dawa za kulevya duniani.

Mwisho wa mwaka jana, Zambada alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Texas akiwa na Joaquín Guzmán López, mtoto wa El Chapo, tukio lililoongeza msukumo wa kufikishwa kwake kwenye vyombo vya sheria vya Marekani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button