Watoto 13 wazaliwa Krismasi Dar

WAKATI waumini wa dini ya Kikristo nchini na duniani wakiendelea kusherehekea Sikukuu ya Krismasi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, watoto 13 wamezaliwa jijini Dar-es-salaam .

HabariLEO ilizungumza na maofisa habari kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Mwananyamala, Agakhan na Hospitali ya Palestina kujua idadi ya watoto waliozaliwa katika usiku huo sambamba na siku ya kuzaliwa kwa Kristo.

Akizungumza na HabariLEO jana, Ofisa Habari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, Florian Godwin amesema katika hospitali hiyo usiku wa kuamkia Desemba 25, walizaliwa watoto watatu, wawili wakiwa ni wa kike na mmoja wa kiume. SOMA: Walindeni watoto ufukweni

Pia, Onesmo Milanzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke amesema katika hospitali hiyo alizaliwa mtoto mmoja wa kike mwenye uzito wa kilo 2.8 na alizaliwa kwa njia ya upasuaji. “Mama pamoja na mtoto wake wanaendelea vizuri chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa hospitali yetu,” alisema Milanzi.

Kwa upande wake Olayce Lotha wa Hospitali ya Rufaa ya Agakhan alisema usiku huo katika hospitali hiyo walizaliwa watoto watano wa kike wakiwa wanne na mmoja wa kiume. Pia, katika Hospitali ya Palestina ilielezwa kuwa watoto waliozaliwa kwenye usiku wa kuamkia sikukuu hiyo walikuwa ni wanne.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I make up to $220 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $450h to $890h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now I am hoping I could help someone else out there by sharing this link.Try it, you won’t regret it!.

    HERE→→→→→→→→→→ https://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button