Mloganzila yatoa huduma upasuaji kurekebisha nguvu za kiume

DAR ES SALAAM; Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma za kibingwa na bingwa bobezi kwa kutoa huduma ya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume(Penile Implant Surgery) kwa wanaume wenye changamoto hiyo ambao hawajafanikiwa kupata nafuu kupitia matibabu mengine.

Akizungumza kuhusu huduma hiyo, Dk David Mgaya, daktari bingwa wa upasuaji wa mfumo wa mkojo na mbobezi wa afya ya uzazi kwa wanaume, amesema tatizo la kupoteza nguvu za kiume linaweza kusababishwa na sababu mbalimbali.

“Kwa vijana linaweza kuhusishwa na changamoto za kisaikolojia, huku kwa watu wazima magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu yakichangia tatizo hilo,” amesema.

Ameeleza kuwa wagonjwa hufanyiwa uchunguzi wa kina ikiwemo kipimo cha Penile Doppler Ultrasound, kinachosaidia kutathmini mtiririko wa damu kwenye uume na kubaini aina ya changamoto iliyopo.

Amesema wanaume ambao hawajafanikiwa kupitia matibabu ya ushauri nasaha, dawa, vacuum device au tiba ya mawimbi (Low Intensity Shockwave Therapy) wanaweza kufanyiwa upasuaji wa kuweka kipandikizi maalumu ndani ya uume (Penile Implant).

” Mgonjwa huhitaji takribani wiki sita kupona kabla ya kurejea katika shughuli za tendo la ndoa,” amesema.

Dk. Mgaya ambaye ni mtaalamu pekee aliyebobea kwenye masuala ya ugumba kwa wanaume hapa nchini ametoa wito kwa wanaume wenye changamoto hiyo kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa uchunguzi, ushauri na matibabu sahihi kulingana na hali zao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button