Mnahesabu lakini pointi za Yanga?

DAR ES SALAAM: MABINGWA watetezi Young Africans wameizidi kutanua uongozi wao wa ligi baada ya kuifunga Singida Big Stars 2-1 katika uwanja wa KMC, Dar es Salaam jioni hii.

Kwa ushindi wa leo, Yanga imekusanya alama 52, wakiwaacha wapinzani wao wa karibu Simba kwa alama 5.

Simba, ambayo itacheza raundi ya 19 na Namungo Jumatano, bado iko katika nafasi ya pili ikiwa na alama 47.

Ili kuuchukua tena uongozi, inawabidi Simba, ambao wana mechi mbili mkononi, kushinda mechi zake zilizobakia ili kufikia michezo 20.

Magoli ya kipindi cha kwanza yaliyopachikwa na Clement Mzize na Prince Dube ndiyo yaliyoamua matokeo katika mechi ya leo.

Mzize ndiye aliyefungua kitabu cha magoli katika dakika ya 13 baada ya kufunga katika piga nikupige iliyotokea karibu na lango la Singida BS.

Zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mapumziko, Prince Dube aliipatia Yanga bao la pili kwa kichwa kufuatia mpira wa kona

Singida Big Stars ndiyo waliotawala kipindi cha pili kwani waliweza kufunga bao la kufutia machozi kupitia kwa Jonathan Sowah katika dakika za majeruhi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button