Mndeme aahidi sera nzuri uwekezaji, ajira kwa vijana

KIGAMBONI, Dar es Salaam: MGOMBEA ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia chama cha ACT – Wazalendo, Mwanaisha Mndeme ameahidi iwapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo, atahakikisha kunakuwa wa sera nzuri ya kuwataka wawekezaji wa viwanda Kigamboni kuajiri kwa wingi vijana.
Mndeme ametoa ahadi hiyo Septemba 13, 2025 katika mwendelezo wa kampeni zake kwenye Kata ya Kimbiji, ambapo alizungumzia changamoto inayowakabili wakazi wa kata hiyo ya miundombinu duni ya barabara inayosababisha ajali za barabarani na ukosefu wa magari ya kutosha ya abiria kuingia na kutoka Kimbiji.

“Nimewahaidi kuwa sauti yao.Nitafanya kazi kwa uongozi shirikishi ili kufikia Kigamboni tunayohiitaji. Kigamboni isiyokuwa na vikwazo vya miundombinu mibovu ya barabara,” amesema Mndeme.
“Pia niligusia suala la ajira kwa vijana, “Jimbo la Kigamboni lina uwekezaji wa viwanda ikiwemo kwenye Kata ya Kimbiji, lakini vijana wa Kigamboni hawanufaiki na fursa hizo za viwanda,” ameongeza.




