Mndeme aishukuru ACT, katibu mambo ya nje

KATIBU mpya wa Mambo ya Nje wa chama cha ACT Wazalendo, Mwanaisha Mndeme amekishukuru chama hicho kwa kuchakuliwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kuitumikia kwa manufaa ya Watanzania.

Jana Machi 8, 2024 Mndeme alichaguliwa kushika nafasi hiyo.

“Napenda kutoa shukrani zangu na shukrani kwa chama changu ACT Wazalendo kwa kuniteua kuwa Katibu wa Mambo ya Nje wa ACT Wazalendo. Nashukuru kwa nafasi hii nzuri na ninayofuraha kubwa ya kuanza safari hii kwa manufaa ya Watanzania wote,” amesema Mndeme.

Advertisement

Mndeme ambaye pia ni mwanasheria, amewahi kuwa Katibu wa Ngome ya Vijana Taifa wa ACT ametoa shukrani hizo mara tu baada ya kushika wadhifa huo.

/* */