Mndeme kuwa sauti ya wavuvi Kigamboni

DAR ES SALAAM: MGOMBEA ubunge Jimbo la Kigamboni, Mwanaisha Mndeme ameahidi endapo atachaguliwa nafasi hiyo, atakuwa sauti ya wavuvi kwa kuhakikisha wanapata vifaa na zana za kisasa.
Sambamba na hilo, Mndeme amewaahidi masoko ya uhakika, uhakika wa hifadhi ya jamii na rasilimali za baharini zinalindwa kwa faida ya vizazi vijavyo.
Mndeme ametoa ahadi hiyo Septemba 19, 2025 katika mwendelezo wa kunadi sera kwa kufanya mkutano wa hadhara Kata ya Kigamboni, Jimbo la Kigamboni.
“Kura yao kwangu ni kura ya kuimarisha maisha ya wavuvi na familia zao na hivyo kuleta maendeleo kwenye jimbo na taifa letu,” amesema Mndeme.