MNRT Saccos yatoa Sh bil 1.2 ya mikopo mwaka mmoja

DODOMA: Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha (MNRT SACCOS LTD) kilicho chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kimefanikiwa kutoa mikopo kwa wanachama wake zaidi ya Sh bilioni 1.2 kwa mwaka kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bernard Marcelline katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa tano (5) wa chama cha MNRT SACCOS LTD uliofanyika katika ukumbi wa TANAPA leo Oktoba 25,2025 jijini Dodoma.

Marcelline amesema kuwa chama hicho chenye wanachama zaidi ya 700 kimewezesha kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi kwa kufanya watumishi kuwa watulivu katika maeneo ya kazi kutokana na uhakika wa kipato.
“Kutoa mikopo ya zaidi ya bilioni 1.2 kwa mwaka maana yake ni fedha zimeingia kwa wanachama na zimekwenda kufanya shughuli za kiuchumi za maendeleo katika sehemu wanazoishi,” amesema Marcelline.

“Nawahimiza watumishi wengine ambao hawajajiunga na saccos wajiunge na sacos hii kwa sababu inakua kwa haraka sana” amesisitiza Marcelline huku akiwahimiza waliokopa kutumia mikopo hiyo kwa malengo waliyojiwekea na pia kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwajengea uaminifu.

Naye, Mwenyekiti wa MNRT SACCOS LTD, Bw. Wilfred Msemo amesema kuwa Saccoss hiyo imefanikiwa kutoa gawio la shilingi milioni 76 kwa wanachama wake, kuchangia katika kuhudumia jamii yenye mahitaji mbalimbali pamoja na kuingiza wanachama wapya 138.




I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website
Open This…. http://Www.Work99.Site
I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
Try it, you won’t regret it!….. https://www.Homeprofit1.site