MOI yagawa viungo bandia bure

ZAIDI ya watu 800 walijitokeza katika zoezi la ugawaji wa miguu na mikono bandia kwa watu wenye uhitaji, lililofanyika chini ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na India.
Akifungua zoezi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dk. Mpoki Ulisubisya, amesoma hotuba ya Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, akiagiza wananchi waliopoteza viungo kujiunga ili kupata huduma hiyo bure inayotolewa na kampuni ya Emcure Pharmaceuticals ya India.
Waziri Mchengerwa amesema upatikanaji wa viungo hivyo bure unawawezesha wahitaji wenye kipato cha chini kurejea katika maisha ya kawaida na kufanya kazi kama awali. SOMA: MOI, India watengeneza miguu bandia kwa Watanzania 600

Balozi wa India nchini, Biswadip Dey, amesema msaada huo ni muendelezo wa ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na India. Aliongeza kuwa hii ni kambi ya pili kufanyika, ikilenga kurejesha utu, furaha na upendo kwa waliopoteza viungo.
Balozi Dk. Mpoki amesisitiza kuwa uchunguzi wa awali utatolewa bure, huku bima ya afya ikitumika tu kwa wahitaji waliyo na bima. Mkurugenzi wa Emcure Pharmaceuticals, Satish Mehta, amesema mpango huu utapanua huduma hiyo hadi vijijini kwa kuanzisha karakana ndogo za utengenezaji wa viungo bandia, ili kupunguza gharama za usafiri kwa wahitaji.
Miongoni mwa wanufaika, Amir Bakari, ameishukuru serikali, MOI na ubalozi wa India kwa kuwezesha upatikanaji wa msaada huu muhimu, akisisitiza kuwa unaleta faraja kubwa kwa maisha yao.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com