Mpanda wahamasishwa usafi wa mazingira

OFISI ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, zimeshiriki kufanya usafi katika soko la Mpanda Hotel, ikiwa ni utekelezaji wa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ya kuwataka wananchi kutenga siku moja kwa wiki kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo,  Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, Sophia Kumbuli, amewataka wananchi kudumisha usafi, ili kuipa hadhi yake Manispaa ya Mpanda.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpanda, Kenneth Pesambili, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph, amesisitiza usafi na utunzaji wa mazingira kuwa ni jadi ya kila mwananchi na kuongeza kuwa kwa ambaye atashindwa kufanya usafi kwa hiyari yake, atakutana na mkono wa sheria.

Mapema wiki iliyopita akiwa katika kikao maalumu kilichohusisha masuala ya afya, lishe na utunzaji wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko aliagiza viongozi wa halmashauri zote mkoani Katavi kusimamia usafi kila Jumamosi, ili kuweka mazingira safi.

Habari Zifananazo

Back to top button