Mpango msibani kwa Katibu Tawala Nzunda

KILIMANJARO – Makamu wa Rais Dk Philip Mapango amesema watumishi wa Umma wanapaswa kumuenzi aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro marehemu Tixon Nzunda kwa kuwa waadilifu, wazalendo na kumtanguliza Mungu katika majukumu yao.

Akizungumza na waombolezaji alipowasili nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Mpango amesema marehemu alikuwa kiongozi na mtumishi wa umma muadilifu na makini katika nafasi mbalimbali alizowahi kuzitumikia serikalini.

Amesema serikali imeguswa na msiba huo na inaungana na waombolezaji wote katika kipindi hiki kigumu. Aidha amewashukuru wananchi kwa kujitoa na kuwa pamoja na familia tangu ilipofikwa na msiba huo.

Dk Mpango amewasihi watanzania kuendelea kuishi vema kazini, kuishi vema na marafiki pamoja na majirani. Amewaasa waombolezaji kupokea msiba huo kama ni mipango ya Mungu na kumuombea marehemu apumzike kwa amani.

Nzunda alifariki dunia jana baada ya kupata ajali wilayani Hai mkoani Kilimanjaro akiwa na Dereva wake.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button