Mpina ataka uchunguzi kuuawa mamba mrefu

DODOMA; Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, ametaka uchunguzi ufanyike kuhusu kutolewa kwa kibali cha uwindaji wa mamba mrefu kuliko wote duniani.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2024/24, Mbunge Mpina amesema Desemba mwaka jana ilipokewa taarifa kuhusu muwindaji mmoja bingwa kutoka Marekani akijitapa akiwa amemning’iza mamba juu ya mti, ambaye ni mrefu kuliko wote duniani akikaribia urefu wa mita tano.

Amesema jambo hilo lilileta taharuki kubwa, lakini katika hotuba ya Waziri hakuliona, pia taarifa kwamba huyo alikuwa mamba mrefu kuliko wote duniani hazikuwahi kukanushwa na taasisi yoyote ndani ya nchi wala nje.

Amesema kama nchi ilikuwa na mamba mrefu kuliko wote duniani, aliruhusiwaje kuwindwa kwa utaratibu wa kawaida na kuhoji Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na TAWA walikubali vipi mamba huyo awindwe.

Isome pia:https://habarileo.co.tz/tawa-aliyeuwa-mamba-alifuata-sheria/

Amesema Tanzania imekuwa ikitafuta vivutio vya watalii na kuhoji kwa nini huyo mamba asingewekewa vizimba na kikajengwa kituo cha utalii, lakini amewindwa kwa kibali cha kawaida tu.

“Naona hizi zilikuwa njama baina ya watendaji wetu wasiokuwa waaminifu kula njama kulihujumu Taifa. Kama haya yamefanyika naomba hatua kali zichukuliwe, lakini uchunguzi ufanyike juu ya jambo hili,” amesema Mbunge Mpina.

Habari Zifananazo

Back to top button