Mradi Shule Bora kuboresha ufundishaji Handeni Mji

MRADI wa Shule Bora upo hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa darasa jipya katika Shule ya Msingi Birikani, Halmashauri ya Mji Handeni, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elieskia Mmbuji, ametoa taarifa hiyo kwa Timu ya Usimamizi ya Halmashauri iliyoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri, Maryam Ukwaju, wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo.

Mmbuji amesema kuwa hadi sasa jumla ya Sh.11,774,310 zimetumika katika hatua mbalimbali za ujenzi, kati ya Sh. milioni 15 zilizopokelewa kutoka Mradi ya Shule Bora mnamo Mei 27, 2025.

 

Ameeleza kuwa ujenzi huo umeanzishwa kwa lengo la kupunguza changamoto ya mrundikano wa wanafunzi na kuimarisha mazingira ya kujifunzia, jambo litakalosaidia walimu kutoa elimu bora zaidi.

“Ukamilishaji wa darasa hili utapunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuboresha mazingira ya kujifunza, hivyo kuongeza ubora wa elimu katika shule yetu,” amesema Mmbuji.

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button