Mradi utafiti wa utamaduni, ubunifu kuzinduliwa Dar

DAR ES SALAAM:Serikali kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Bora Initiative inatarajia kuzindua mradi mpya wa utafiti unaoitwa Connect for Culture Afrika(CfCA) utakaohusisha eneo la utamaduni na ubunifu nchini ili kufanya tathmini ya mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam Naibu Mkurugenzi Mteandaji wa Tanzania Bora Initiative,Ismail Biro, amesema mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa Agosti 22,2025 ambapo moja ya maeneo watakayojikita kwa kushirikiana na serikali watahakikisha wanwajengea uwezo wasanii.

“Licha ya kuwajengea uwezo lakini pia kuna ufinyo wa taarifa na tafiti zinazoelezea hali ya sekta imefanya sekta hii kuonekana isiyo rasmi hivyo tutajikita katika kufanya tafiti ambazo zinaelezea hali ya sekta na mchango wa sekta katika pato la taifa.

“Lakini pia tutajihusisha na mamlaka zingine ili waweze kutumia hizo tafiti na kutumia taarifa hizo katika kufanya maamuzi na tunataraijia viongozi watashiriki katika mijadala katika ukanda waAfrika kwani inafanyika sehemu zingine za Afrika ,”amesisitiza.

Amesema wanataka vijana kuona ajira rasmi katika sekta hiyo na kuchangia maendeleo ya nchi kwa kuongeza pato ambapo mradi huo pia una lengo la kuwepo kwa uwekezaji wa asilimia moja kwa sekta za umma.

Biro amesema mradi huo wa miaka mitano hadi 2030 utahusisha nchi nzima na wataendana na mwaka wa serikali ili kuendana na mipango ya serikali.

Kwa upande wake wakilishi wa Mkurugenzi wa idara ya utamadunia wizara ya utamaduni na michezo,Mfaume Said amesema serikali imekuwa ikitafuta taarifa kwa muda mrefu zitakazowezesha kuboresha sekta ya utamaduni na ubunifu, hivyo kuja kwa mradi utasaidia kujua kama wizara wapi wataenda kuboresha.

“Sera ya utamaduni inaelekeza ushirikiano na wadau mbalimbali kwani serikali haiwezi kufanya kila kitu, mradi huu unaenda kuangazia takwimu zilizopo katika sekta hiyo hasa wadau wanapata kipato gani na changamoto zao hii iturahisishia kwenye mipango.

Amesema hivi sasa wako kwenye mkakati wa utekelezaji wa sera ya utamaduni na wako mbioni kuihuisha sera ya utamaduni ya 1997 hivyo utafiti huo utawasaidia mambo muhimu ya kuzingatia.

Naye Beatrice Waruinge, Ofisa Programu (CfCA) kutoka Shirika la SELAM ambayo inashirikiana na Tanzania Bora Initiative kutekeleza mradi huo amesema shirika lao limekuwa likiendelea kuhamasisha utekelezaji katika sekta ya utamaduni na ubunifi kwa ukanda wa Afrika.

“Mradi huu unalenga kuimarisha uwezo,uendelevu na mwaonekano wa sekta ya sanaa na utamaduni wa Tanzania sambamba na kujenga ushirikiano thabiti kati ya serikali,wadau wa maendeleo,sekta binafsi na watendaji wa ubunifu,”amesema.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button