Msando aihakikishia Ubungo amani Oktoba 29

DAR ES SALAAM: WAFANYABIASHARA wa Wilaya ya Ubungo wamehakikishiwa uwepo wa amani Oktoba 29, siku ya uchaguzi na kwamba baada ya kupiga kura waendelee na biashara zao.
Aidha, kuelekea uchaguzi huo, wananchi wa wilaya hiyo, na kwengineko wameonywa kutojihusisha na maandamano.
Akizungumza kwenye Kongamano la Vikoba mapema leo Oktoba 29, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kuwa wilaya hiyo itakuwa na amani kabla na baada ya zoezi la kupiga kura.
“Huyo mtu anaenda kuandamana ili iweje, watanzania si hawa hapa, kama wamechoka na amani mbona wako hapa,” amesema Msando.
Akizungumzia suala la vikoba , Msando amesema serikali ina nia ya dhati wananchi wote waliojiunga vikoba wanawezeshwa kiuchumi.
“Kuwawezesha wananchi ni jukumu la serikali, kama mnavyofahamu, jukumu la msingi kwa mujibu wa katiba ni huduma za jamii,” ameeleza Msando.