Msimamizi wa uchaguzi aeleza kuhusu mawakala Chadema

MSIMAMIZI wa Uchaguzi Halmshauri ya  Jiji la Arusha, John Kayombo amesema Chama cha Demokrasia  na Maendeleo ( CHADEMA ) kimepeleka mawakala zaidi ya watatu katika baadhi ya vituo na haijulikani wanania gani.

Lakini pia  baadhi ya maeneo wagombea wa chadema wanataka kuwa mawakala katika baadhi ya vituo lakini kanuni hazipo hivyo

Kayombo ameyasema hayo  leo wakati akioongea na wanahabari katika shule ya Sekondari Olorien kata ya Olorien jijini Arusha

Advertisement

Amesema mgombea hawezi kuwa wakala labda anaweza kuwa wakala katika kituo cha majumuisho na aweameapishwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi

Kayombo amesema baada ya kueleimishwa chadema wameleta mawakala wasaidizi kwa ajili ya kusimamia zoezi hilo lakini zoezi hilo la upigaji kura linaendelea vema

“Sijapata malalamiko yoyote ya chadema na uchaguzi unaendelea vema,wananchi wanapiga kura na kuondoka zao, wananchi wanataka maendeleo na Chadema kama wanaushahidi wa kura kujaa kwenye maboksi watoe maana kabla ya uchaguzi maboksi yanaonyeshwa na yanafungwa sasa hizo changamoto zao wanatoa  wapi”

Amesema jiji la Arusha limeandikisha wananchi zaidi ya 389,000 hivyo wananchi wasome vizuri majina yao kwenye ubao wa matangazo na wakishindwa kuyaona daftari lipo linaonyesha majina yao.