Msongamano wa wagonjwa wapungua hospitali wilaya ya Geita

GEITA: HALMASHAURI ya Wilaya ya Geita mkoani Geita imepokea na kutumia kiasi cha fedha sh 893.43 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Geita.

Kaimu Mganga Mfawidhi na Mfamasia wa Hospitali hiyo, Dk Simon Kalumanga ameeleza hayo Septemba 01, 2025 wakati akisoma taarifa ya mradi huo kwa viongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2025.

Dk Kalumanga amesema mradi huo unahusisha wodi ya wanawake, wodi ya wanaume na wodi ya watoto katika hospitali hiyo ambapo ujenzi upo kwenye hatua za mwisho kwa ajili ya kuruhusu

Amesema kati ya pesa hiyo kiasi cha Sh milioni 500 ni fungu kutoka serikali kuu huku sh milioni 393.43 ni pesa ya uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) kutoka Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) 2022/2023.

Amesema utekelezaji wa mradi ulianza Machi 2021, kwa utaratibu wa Force Account ambapo kupitia utaratibu huo, halmashauri ilikuwa na jukumu la kuajiri mafundi ujenzi na kusimamia zoezi zima la ununuzi wa vifaa.

Anesema katika kuhakikisha ubora wa kazi kupitia kamati za manunuzi, mapokezi na ujenzi kwa fedha kutoka Serikali kuu na ukamilishaji kwa kupitia GGML ilikamilisha Mradi kwa mfumo wa kuajiri mkandarasi.

DK Kalumanga amefafanua kuwa mpaka kukamilisha mradi, wodi ya Wanawake iligharimu sh milioni 321.12, wodi ya wanaume ilitumia kiasi cha sh milioni 265. 42 na wodi ya watoto imegharimu sh milioni 306.88.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2025, Ismail Alli Ussi amehimiza viongozi wa serikali kusimamia huduma stahiki kwa wodi zilizojengwa ili kufanikisha azma ya serikali kupunguza msongamano katika wodi.

Aidha Ussi amewataka viongozi kujenga mazingira rafiki ya wananchi wote kupata taarifa ya miradi hiyo ili kusaidia jamii kupata uelewa wa miradi inayotekelezwa na serikali kufanikisha utawala wa mfumo shirikishi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button