Mtemi wa Wagogo adai ana uwezo wa kuita mvua

MTEMI Yassin Biringi wa Dodoma Makulu, amedai miongoni mwa vitu alivyoachiwa ni mawe ya tambiko yanayotumika kuita mvua pale zinapochelewa, pia ana uwezo wa kusimamisha mvua.

Akizungumza leo wakati wa mahojiano, alisema Machifu Wana nguvu za asili za kufanya mambo yakatokea

Biringi  ni Mtemi wa kabila la Wagogo, aliapishwa hivi karibuni na kurithi mikoba ya baba yake..

“Nina uwezo wa kusimamisha mvua na hili huwa nalifanya nikiwa na mavazi maalum na kuna maneno huwa natamka,” alisema na kuongeza kuwa, jamii ya sasa ni ngumu sana kuamini mila na tamaduni za asili.

Alisema kuwa amechaguliwa kuwa Mtemi wa kumrithi baba yake, Ali Biringi ambaye sasa ni mgonjwa.

“Mzee sasa ana miaka 84, ana watoto 57 kwa wake wanane, ambapo mimi ni mtoto wa 27 sasa, nina miaka 32,” alisema na kuongeza kuwa baba yake ana wajukuu 127, vitukuu 98 na vilembwe 57.

“Mtoto wake wa mwisho ana miaka minane, kwa sababu ya ugonjwa ndio maana hana tena watoto wengine wadogo,” alisema

“Zamani Chifu yoyote ni lazima aoe wanawake wengi  kwa sababu shughuli za uchifu ni nyingi na hupokea wageni wengi, lazima kuwe na watu wa kumsadia kumudu majukumu mengine kama ya kilimo na ufugaji,” alisema.

Alisema Mteni anapatikana kwenye familia haangalii mtoto mkubwa au mdogo, lakini lazima achaguliwe.

“Kuna wazee wa mila, mizimu yenyewe ikuchague ukikubali mzee mwenyewe ndio anaelekezwa na mizimu, akilala anaoteshwa mtu atakayekalia kiti chake ni huyu, baadaye wanakuja  kukusimika, licha ya kuchaguliwa uwe na hekima na busara na moyo wa utu ndipo utapewa,” alisema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button