MtumiajiApp kuboresha huduma za mawasiliano

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amezindua mfumo wa kidijitali wa kuwahudumia watumiaji wa huduma za mawasiliano unaojulikana kama MtumiajiApp, ulioandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kairuki amesema mfumo huo ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za mawasiliano nchini. Amefafanua kuwa MtumiajiApp utawasaidia watumiaji kupata taarifa muhimu, kuelimishwa kuhusu matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano, pamoja na kutoa fursa ya kuwasilisha changamoto na maoni yao.

Kairuki amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa Kidijitali 2024–2034, uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi ya teknolojia na kuhakikisha wananchi wanatumia mifumo ya kidijitali kwa usalama na ufanisi.

Kwa mujibu wa takwimu za TCRA, idadi ya laini za simu nchini ilifikia milioni 106.9 hadi Desemba 2025, huku watumiaji wa intaneti wakifikia milioni 58.6, hali inayonyesha ukuaji wa haraka wa sekta ya mawasiliano. SOMA: SADC yazindua Mkakati wa Mawasiliano 2025/2030

Aidha, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), ambapo minara 758 imejengwa na kufikisha huduma katika zaidi ya vijiji 1,400, hatua iliyowawezesha wananchi wengi kupata huduma hata katika maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara.

Pamoja na mafanikio hayo, Kairuki alitaja changamoto zinazokabili sekta ya mawasiliano kuwa ni pamoja na uelewa mdogo wa watumiaji, uvunjifu wa faragha, na vitendo vya utapeli mtandaoni. Amesema mfumo wa MtumiajiApp utasaidia kushughulikia changamoto hizo kwa kutoa njia rahisi kwa watumiaji kuwasiliana na wadau husika.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button