Mtwara Mikindani wazawadia Shule zilizong’ara 2025

MTWARA; MANISPAA ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imetoa zawadi kwa shule 15 za msingi zilizofanya vizuri matokeo ya darasa la saba mwaka 2025.
Tukio hilo limefanyika wakati wa kikao kazi kwa wakuu wa shule, maofisa elimu kata pamoja na wataaluma wa manispaa kilichofanyika kwenye manispaa hiyo.
Zawadi zilizotolewa ni fedha taslimu taslimu Sh milioni 6 zitakazogawanywa kwa walimu 30 wa shule hizo 15, ambapo kwa kila shule ni mwalimu mkuu na mwalimu wa taaluma.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawahi hiyo, Mkurugenzi wa manispaa hiyo Mwalimu Hassan Nyange amesema lengo la kikao ni kujiwekea mikakati ya kitaaluma katika idara elimu msingi kwa mwaka wa masomo 2026, huku akiwataka walimu hao kutobweteka na mafanikio hayo.

“Tusibweteke na mafanikio haya badala yake tuweke mikakati madhubuti zaidi ya kuboresha matokeo ya mitihani kwa mwaka 2026,”amesema Nyange.
Amezitaja shule zilizofanya vizuri kuwa ni Heritage, King David, Michael Angel, Medi, Salem, Shangani, Kambarage, Maendeleo, Mangamba, Rahaleo, Mtawanya, Namayanga, Muungano, Ligula na Mnaida.




Good article. I’m dealing with some of these issues as
well..