Muhimbili kuanza kuhifadhi mbegu za uzazi

DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua benki ya kuhifadhi mbegu za uzazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel akizungumza leo Februari 28, 2024 amesema Rais Samia atazindua benki hiyo hivi karibuni.

Amesema MNH imeanza kuhifadhi mbegu hizo za uzazi na mtu akitaka kupata mtoto basi atafika hospitalini hapo na kupandikiziwa.

“Mbegu zitahifadhiwa kwa muda wa miaka mitano hadi 10, mtu kama hahitaji mtoto kwa wakati husika zitahifadhiwa, wakati akiona sasa anahitaji kupata mtoto basi atapandikiziwa,” amesema.

Amesema sio lazima watu waende nje kupandikiza kwani ndani ya hospitali hiyo wanapandikiza na kutunza mbegu hizo.

“Sio lazima uende Uturuki kupandikiza mimba, Muhimbili tunafanya na kama ukihitaji kuhifadhi mayai yako hutaki mtoto kwa sasa hadi hapo baadae tunakuhifadhia mayai yako hadi hapo baadae utakapokuwa tayari tutalikutanisha na kupata mtoto,”amesema Dk Mollel .

 

Habari Zifananazo

Back to top button