Muhimbili yaja kivingine upatikanaji wa dawa

DAR ES SALAAM: Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), leo imesaini mkataba wa makubaliano na kiwanda cha Kairuki KPTL kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa dawa Muhimbili upanga na Mloganzila.
Mkataba huo umeanisha maeneo mawili,Kuboresha upatikanaji wa dawa ambazo hazipatikani kwa urahisi kwenye soko ikiwemo zinazotumika katika upandikizaji wa viungo mbalimbali mwilini kama Figo,Kongosho pamoja na dawa zenye ujazo mdogo zinazotumika kwa watoto na wagonjwa wa saratani.
Eneo la pili la makubaliano ni kuwajengea uwezo wataalamu wa Muhimbili katika uzalishaji wa dawa na namna ya kuongeza kuzitumia dawa zinazozalishwa na kiwanda hicho.
Mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema hiyo ni hatua nzuri kuwepo kwa kiwanda cha dawa ambacho kinamilikiwa na wazawa na kukidhi viwango vinavyohitajika.
Pia, amefafanua kuwa Muhimbili ni hospitali ya Rufaa ya kitaifa ni kubwa kuliko zote nchini ina vitanda 2,150 ambapo upanga kuna vitanda 1,550 na Mloganzila kuna vitanda takribani 600 hivyo inawahudumia wengi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha dawa cha Kairuki Dk.Muganyizi Kairuki amesema kiwanda hiko kimedhamiria kuzalisha bidhaa kulingana na mahitaji yaliyopo na kuhakikisha mkataba uliopo unakuwa na tija kwa hospitali.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
18 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Lorrainemith
Lorrainemith
18 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 18 days ago by Lorrainemith
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x