Mvomero wafanya kweli mikopo asilimia 10

HALMASHURI ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro imekamilisha awamu ya kwanza ya utaratibu wa utoaji wa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 670.9 kwa ajili ya vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu vilivyokidhi vigezo.

Mratibu wa Mikopo Wilaya ya Mvomero, Mashaka Malole amesema hayo  kabla ya Mkuu wa wilaya hiyo, Judith Nguli kuzindua utoaji wa mikopo hiyo kwa vikundi 79 vinavyotoka katika kata za tarafa ya Turiani, Mvomero, Mgeta na Mlali.

Malole amesemakuwa kati ya vikundi hivyo ,58 ni vya wanawake ambavyo kumepatiwa jumla y ash milioni 400.4 vikundi vya vijana 17 vilivyonufaika na jumla y ash milioni 218.5 pamoja na vikundi vinne vya watu wenye ulemavu ambayo vimepatiwa jumla ya Sh milioni 24.

Advertisement

Naye Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Saidi Nguya  ambaye ni Mwenyekiti wa Uratibu wa Mikopo hiyo amesema  ,timu yake ya uhakiki ilitembelea vijiji vilivyokuwa na vikundi na kuridhia vimekidhi vigezo kupata mikopo hiyo  katika awamu ya kwanza utoaji wake.

“ Hatukutaka tukee mezani na kusubiri ripoti, tulikwendakatika kila kijiji ambako kuna kikundi kimeomba kupewa mkopo ili  kukihakiki kujiridhisha endapo kimekidhi vigezo vya kupata mkopo huu” amesema  Nguya.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Nguli amesema Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikiwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutambua kuwa ni chachu ya Maendeleo kwa Taifa.

Mbali na hayo aliwatahadharisha wanufaika na mikopo hiyo kuwa halitakiwi kutoa rushwa kuanzia ngazi ya chini hadi juu.

Amewataka  walengwa wa mikopo hiyo kutoa taarifa kwake ama Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya pale watendaji watakapowa omba kitu chochote  ili wawezechukuliwe hatua za kisheria dhidi yao.

“ Nimeambia kuwa watu wanaweza kuwa na tabia zile sio nzuri za kuzuia haki zao …niwaambie neno moja zoezi hili halitakiuoe kitu chochote …zoezi la utoaji wa mikopo halitaki rushwa kuanzia chini hadi  juu, kinachoangaliwa ni kigezo pekee” amesema Nguli.

Mkuu wa wilaya amewataka wanufaika wa mikopo  hiyo kuifanyia kazi kulingana na mipango na malengo yake ikiwa  na kuhakikisha wanairejesha kwa wakati iweze kuwanufaisha na wengine.