Mvua ziongeze uzalishaji kilimo – Batilda

TANGA: MKUU wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Burian, amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Handeni kutumia fursa ya mvua zinazoendelea kunyesha kufanya shughuli za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha kipato cha familia.

Wito huo ameutoa wakati wa hafla ya Iftar maalumu iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Salum Nyamwese, iliyowakutanisha viongozi wa dini pamoja na wananchi mjini Handeni.

Mkuu wa Mkoa huyo amewataka wananchi kutumia kipindi cha mvua kufanya shughuli za kilimo kwa bidii ili kujihakikishia usalama wa chakula pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao.

Aidha, amewakumbusha wananchi umuhimu wa kuendeleza mshikamano na kufanya matendo ya huruma, hususan katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani tunapoelekea katika sikukuu ya Eid al-Fitr.

“Tunapoelekea katika sikukuu ya Eid ni muhimu kuendelea kushirikiana na kusaidiana, kuwajali wenye uhitaji na kuimarisha upendo katika jamii,” amesema.

Katika kuonesha mshikamano na wananchi wa Handeni, kiongozi huyo pia amechangia Sh milioni 1 kama mkono wa sikukuu ya Eid kwa ajili ya kusaidia wananchi wenye uhitaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Salum Nyamwese, amesema Iftar hiyo imelenga kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano kati ya viongozi wa serikali, viongozi wa dini na wananchi ili kuendeleza amani na maendeleo ya wilaya hiyo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button