Mvuvi asimulia baada ya kuokoa saba Precision air

HASHIMU Rashidi mvuvi na mkazi wa Nyamukazi Mwaloni ameokoa abiria saba (7) waliokuwa katika ndege ya Precision air iliyopata ajali mapema jumapili na kuanguka katika Ziwa Victoria, mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba.

Anasema haikuwa rahisi kwa kuzingatia wavuvi hawakuwa na vifaa wala elimu sahihi ya uokozi. Shuhuda huyo wa ajali ya ndege ameeleza kuwa alishuhudia ndege ikikaribia kutua uwanjani hata hivyo alishtushwa na kishindo majini.

“Niliwasha boti haraka na kuelekea katika ndege. Abiria walifungua mlango wa dharura lakini hakuna aliyesema chochote kwa hofu,” alisema Rashidi.

Kwa mujibu wa Rashidi kati ya abiria saba aliookoa, mmoja alikuwa mama ambaye alionekana kuumia sehemu ya mguu.

Mkuu wa Mkoa wa Kagara Albert Chalamila amesema abiria 26 kati ya 43 walio okolewa wanaendelea na matibabu.

 

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button