DAR-ES-SALAAM: Mwimbaji wa Nyimbo za Injili nchini,Boniface Mwaitege amekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa yeye amefariki.
Akikanusha taarifa hiyo kwenye mitandao ya kijamii, Mwaitege amesema anashangaa kuona watu wanaandika taarifa ambazo sio sahihi na kudai kuwa yeye mzima na wala hajafariki.
Pia amewaomba mashabiki wake kupuuzia taarifa hiyo ambayo haina ukweli wowote bali ni kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii ama wanataka kupata wafuasi wengi kweney mitandao yao.
“ndugu zangu mnaonitazama niko mzima, mwenye afya kama mnavyoniona sijapata ajali yoyote sina tatizo lolote ni uzushi tu kwahiyo naomba kama unanisikia nisaidie kufikisha taarifa hii kwa wengine ili kujaribu kushusha presha ya uzushi huu ambayo bado sijajua chanzo nini”, alisema Mwaitege