Mwakinyo msimamo ni uleule,

DAR ES SALAAM: BONDIA Hassan Mwakinyo amesema ana asilimia 5% tu za kupanda ulingoni kwenye pambano lililopangwa kupigwa leo septemba 29, 2023 la kuwania mkanda wa IBA na mpinzani wake Julius Indongo
Kupitia mitandao yake ya kijamii Mwakinyo ameandika…
“Maswali na simu zimekuwa nyingi, kiukweli mpaka sasa nina asilimia 5 tu za kupanda ulingoni ikiwa zitaongezeka ni mimi mwenyewe nitasema, naomba tuwe wavumilivu , epuka matapeli msimamo ni mmoja tu kama mogadishu… kwa kitendo hiki naomba huu ndio uwe mwisho wa mapromota dhuluma wadanganyifu na matapeli…” amendika Mwakinyo
Ikumbukwe jana mwakinyo aliandika kwenye mitandao yake kuwa hatoweza kupambana kutokana na Udanganifu wa Mapromota na mpaka sasa wapenzi wa masumbwi wapo njiapanda juu ya uwepo wa pambano hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button