Mwakinyo: Nina asilimia 5 kupanda ulingoni

DAR ES SALAAM: BONDIA Hassan Mwakinyo amesema ana asilimia 5 tu za kupanda ulingoni kwenye pambano lililopangwa kupigwa leo Septemba 29, 2023 kuwania mkanda wa IBA na mpinzani wake Julius Indongo

Kupitia mitandao yake ya kijamii Mwakinyo ameandika: “Maswali na simu zimekuwa nyingi, kiukweli mpaka sasa nina asilimia 5 tu za kupanda ulingoni ikiwa zitaongezeka ni mimi mwenyewe nitasema.

“Naomba tuwe wavumilivu , epuka matapeli msimamo ni mmoja tu kama Mogadishu… kwa kitendo hiki naomba huu ndio uwe mwisho wa mapromota dhuluma wadanganyifu na matapeli,” amendika Mwakinyo

Ikumbukwe jana mwakinyo aliandika kwenye mitandao yake kuwa hatoweza kupambana kwa madai ya udanganifu wa mapromota na mpaka sasa wapenzi wa masumbwi wapo njiapanda juu ya uwepo wa pambano hilo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
money
money
2 months ago

Mashindano ya nani kuhinda kwenye neno “ABROAD“ NCHINI TANZANIA!?

MJERUMANI

MHINDI

MTANZANIA

MKENYA

MNIGERIA

MHISPANIA

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg

NANI AINGIZE NDEGE ZA KWENDA KUMSALIMIA BABU NA BIBI, KWA ALIYESHINDA KULELEWA NA BIBI TU!?

Capture.JPG
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x