Mwanachama mpya CCM avamiwa

PEMBA : CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria kwa watu wote waliohusika na vitendo vya kuchoma moto mali za mwanachama mpya wa CCM kutoka ACT-Wazalendo Salum Mohamed Juma katika shehia ya Wingwi Mapofu Wilaya Micheweni Pemba.

Amesema baadhi ya wanachama wapya wa CCM wameanza kutishwa na kufanyiwa vitendo vya hujuma na wengine kujeruhiwa na kuharibiwa mali zao hali inayotakiwa kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Akiweka jiwe na msingi katika maskani ya CCM mjini Kiuyu Jimbo la Kojani, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa amesema watu wasiojulikana wamevamia makaazi ya mwanachama mpya wa CCM aliyekuwa ACT-Wazalendo Salum Mohamed  na kuingia nyumbani kwake wakachoma moto godoro,vitambulisho,nguo na bendera ya CCM kisha kukimbia baada ya wananchi kujitokeza kuzima moto uliokuwa umeanza kuchoma makaazi ya mwanachama huyo.

“Chama Cha Mapinduzi tuna dhamana ya kulinda amani na utulivu wa nchi kwa gharama yoyote hatuwezi kukubali Zanzibar irudi katika siasa za chuki na machafuko kwa Wananchi wasiokuwa na hatia,”alisema  Dimwa

 

SOMA : CCM YATOA KAULI KIFO CHA KADA CHADEMA

Habari Zifananazo

Back to top button