Mwanafunzi amuua mwenzake kwa kichapo Geita

MWANAFUNZI wa darasa la pili katika shule ya msingi Uwanja iliyopo kata ya Nyankumbu mjini Geita, Jovina Simon (10) amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kupigwa meteke tumboni na mwanafunzi mwenzie.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Ally Kitumbu amethibitisha tukio hilo alipozungumuza na waandishi  wa habari na kumtaja mtuhumiwa wa tukio ni  kwa ni mwanafunzi wa darasa la saba, shule ya msingi Mkombozi iliyopo mjini Geita, Haruna Amin (16). 

Ameeleza, tukio hilo limetokea Agosti 25, 2022 majira ya saa saba mchana katika mtaa wa Elimu mjini Geita wakati Jovina na Haruna walipokuwa wakigombana na ndipo Haruna alipompiga teke tumboni na kumsababishia Jovina maumivu makali ya tumbo.

“Jovina alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, siku hiyo  hiyo ya Agosti 25 na kwa bahati mbaya alifariki dunia Agosti 29, 2022  majira ya saa 12 asubuhi. 

“Hadi sasa mwili wa marehemu unaendelea kuhifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” amesema.

Akizungumuzia tukio hilo, baba mzazi wa Jovina, Simon John amesema siku ya tukio hakuwepo nyumbani bali alipigiwa simu na mkewe  kuwa mwanae (Jovina) ameumia kwa kupigwa na mtoto mwenzie ambaye ni mtoto wa jirani.

“Nilirudi nyumbani baada ya mke wangu kunipa taarifa hiyo nikawakuta wako hospitali tayari, alipatiwa matibabu siku ya kwanza, ya pili na ilipofika Agosti 29, 2022 alifariki. Sijajua chanzo Cha ugomvi wao  ila huyo mtoto ni jirani yangu wa chumba cha pili.

“Kipindi namuuguza hospitalini alisema mwenzie alimpiga na teke na ngumi chini ya ubavu. Baada ya kupima  vipimo vya X-Ray daktari alituambia amepigwa sehemu mbaya na bandama imeharibika vibaya na ndicho kilichopelekea kifo chake.’ Amesema baba wa marehemu.

 

Habari Zifananazo

Back to top button