Mwanga Benki yaanza huduma mpya ya mikopo

DAR-ES-SALAAM : BENKI ya Mwanga Hakika imezindua huduma mpya ya utoaji haraka wa mikopo kupitia hati fungani inayoitwa ‘Mkopo Chap’ ili kurahisisha upatikanaji wa haraka wa fedha kwa wawekezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Meneja wa Wateja wadogo na Wateja wa kati wa Mwanga Hakika benki,Mwinyimkuu Ngalima amesema Mkopo Chap unatolewa kwa wale ambao wanahati fungani ambapo inaweza kuwa ni bond au vvipande mfano vipande vya UTT na vingine zote zinahusika katika utoaji wa mkopo huo.
“Siku ya leo tumezindua bidhaa nzuri kwa wawekezaji na tumeona kuna haja ya kutoa suluhu kwa waliowekeza kwenye hati fungani lakini wanahitaji msaada kidogo wa mahitaji wa kifedha Hakika imekuja na Mkopo chap.
Ameongeza “Kwahiyo mkopo chap mtu anaweza kupata kwa haraka sana ambapo atatuonesha yeye anahati fungani ya kiasi gani na thamani ya hizo hati fungani huwa tunaangalia moja kwa moja ziko wazi unaangalia kwenye website wanatoa.
Amesisitiza kuwa kwa wale wawekezaji wote hata wakiweka hisa tunazipata kwenye hayo maeneo na hata kwa wale wenye vipande kuna wale wanaitwa funding manager mfano kama TIMIZA na wengine hizo thamani zinapatikana.
Aidha ameeleza kuwa mkopo huo unachukua ndani ya muda mfupi sana ambapo ni siku tatu hadi nne na jambo wanalofanya ni kuongeza uwezo wa Mwanga Hakika Benki kwenye hati fungani yako.
“Utajaza fomu chache pale benki tutakupa hadi asilimia 80 ya thamini ya uwekezaji wako ila tujue tu ni uwekezaji wa aina gani,na mkopo huo tumeweka uwe rahisi kwa malipo inategemea wewe ulipe kiasi gani na kwa muda gani kwamaana unaweza kulipa kila mwezi,kila baada ya miezi mitatu hata miezi sita tunaruhusu,”amefafanua.
Ngalima amesema kuwa mkopo huo pia umeletea fursa kwani hatifungani kwa Mwanga Hakika Benki inaweza kutumia kwa mikopo mingine.
“Unaweza kuja na ukataka kununua gari kwa hatifungani yako na tukakupa mkopo tukakubaliana unalipaje ,hayo yote inatokana na jitihada ya Hakika kutafuta suluhisho la changamoto ili kuhakikisha mwekezaji asiwe na stress tena akipata changamoto ya uwekezaji
Afisa Mkuu wa soko la hisa Dar es Salaam, Peter Nalitolea amesema mikopo hiyo inatumia hati fungani ,hisa au vipande kwa uwekezaji kutumia kama dhamana kwenda kukopa hivyilo wamekuja na bidhaa mpya kabisa kutumia hati fungani za makapuni.
Amesema kutokana na huduma hiyo mwekezaji hahitaji kuuza ukwasi wake akiwa na uhitaji bali atakuja kuchukua mkopo huvyo inafaida kwenye soko itafanya soko kuendelea kukua na kuongezeka. SOMA: Z’bar yazindua hatifungani ya Kiislamu ya kwanza EAC
“Kama mwekezaji akiona kuwekza hakunizuii kupata hela ya haraka haraka basi akiona kesho anahitaji kitu cha haraka haraka atafanya hivyo akihitqji hela ya matibabu anaweza kukopa kwa muda mfupi,”amesisitiza.
I am now making an extra $19k or more every month from home by doing a very simple and easy job online from home. sxs I have received exactly $20845 last month from this home job. Join now this job and start making extra cash online by following the instructions on the given website………………….. Www.JoinSalary.Com