Mwangaza sheria ya mtoto kudhibiti ukatili

GEITA: UELEWA duni pamoja na kupuuzwa kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009 miongoni mwa wazazi, walezi na taasisi imetajwa kuwa kiini kikubwa cha ongezeko la matukio ya ukatili dhidi ya watoto mkoani Geita.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Geita, Paulina Majogoro amesema hayo katika mahafari ya 11 ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya Geita Adventist iliyopo mjini Geita.

Amesema changamoto hiyo inaashiria kuna uhitaji mkubwa wa elimu na msisitizo wa sheria ya mtoto kwenye familia na jamii ili kuimarisha usalama na usimamizi wa ulinzi wa kisheria wa haki ya mtoto.

Ameeleza, wapo wazazi wanaamini mtoto anapohitimu elimu ya msingi ama sekondari yupo tayari kujitegemea ingali ana umri chini ya miaka 18 na kupelekea watoto wengi wa kike kuwa hatarini zaidi.

“Jukumu la kwanza la wahitimu ni kwenda kuyaishi yale waliyolelewa na yale waliyofundishwa, jukumu la pili ni wazazi bado wanayo nafasi ya kutoa elimu ya kuendeleza maadili kwa watoto wao.

“Wasiwaache watoto holela eti kwa sababu wamemaliza kidato cha nne, lakini jukumu la tatu bado ni la jamii nzima kuhakikisha watoto wetu hawa wanaokuja basi wanakuwa kwenye mazingira salama.

“Kwa hiyo tujitahidi kama jamii tunashirikiana pamoja tunapambana hii vita ya kuwalinda watoto wetu ya kuhakikisha wako salama na hili jukumu siyo la mtu mmoja ni la wazazi, walimu, serikali na kila mtu.”

Mkurugenzi wa Shule za Geita Adventist, George Hezrone amesema jumla ya wanafunzi 234 wamefanya mahafari ya kuhitimu kidato cha nne ambapo wamejengwa zaidi katika elimu ya kidini na kitaaluma.

Amesema pia shule za Geita Adventist zimewekeza kuwafundisha watoto haki zao ili wapate ufahamu na ujasiri wa kujilinda dhidi ya viashiria na vitendo vya ukatili wawapo shuleni, nyumbani na mtaani.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Virginiallen
Virginiallen
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by Virginiallen
Julia
Julia
1 month ago

I’m making a good salary from home 16,580-47,065/ Dollars week, which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. I was blessed with these instructions and now it’s my duty to pay it forward and share it with everyone.
.
.
Detail Here————————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

Marry
Marry
1 month ago

★I am making a real GOOD MONEY (123$ / hr ) online from my laptop. Last month I GOT check of nearly $30k, this online work is simple and straight forward, don’t have to go OFFICE, Its home online job.(nfa) You become independent after joining this JOB. I really thanks to my FRIEND who refer me this SITE. I hope you also got what I…go to home media tech tab for more detail reinforce your heart…
══════HERE► http://Www.Smartcareer1.com

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x