Mwanza kwenye mikakati ya kumtua Mama ndoo ya maji kichwani

MWANZA: Katika kuhakikisha huduma ya maji Jijini Mwanza inaimarika, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imepokea shehena ya mabomba yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.4 kwa ajili ya maeneo ya Buswelu, Nyamadoke na Kahama.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya shehena hiyo ya mabomba Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Neli Msuya amesema kuwa MWAUWASA inatekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwenye maeneo inayohudumia ili kuwapunguzia adha wananchi sambamba na kufikia azma ya Serikali ya kumtua Mama ndoo ya maji kichwani.
“Hii ni shehena ya kwanza na tunatarajia siku mbili zijazo tutapokea shehena nyingine kwa ajili ya maeneo ya Luchelele, Ilalila na Kisesa,” ….Amesema
Msuya ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maji kwa jitihada zake za makusudi za kuimarisha huduma ya maji Mwanza.
Tunaishukuru Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dk. Suluhu Hassan kupitia Waziri wetu wa Maji, Jumaa Aweso kwa kujitoa kwa ajili ya wananchi wa Mwanza, kuhakikisha wana Mwanza wanapata huduma ya majisafi na salama,” amesisitiza
Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Diwani wa Kata ya Buswelu Sarah Ng’wani ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma ya maji Jijini Mwanza.Vna kuwasihi wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu ya maji.