Mwanza wahimiza uchaguzi wa amani

Zikiwa zimesalia siku nne kufanyika kwa uchaguzi mkuu, Oktoba 29, 2025, makundi mbalimbali yamekusanyika mkoani Mwanza kuhimiza wananchi kujitokeza huku wakizingatia utunzaji amani.
Ni mkusanyiko uliofanyika leo Oktoba 25,2025 katika uwanja wa Nyamagana kupitia ‘Kongamano la Amani Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025’, ukihusisha pamoja na makundi mengine, watu wenye ulemavu, mama lishe, wafanyabiashara wadodo, pamoja na madereva wa vyombo mbalimbali vya usafiri wa umma.
Mwenyekiti wa waendesha pikipiki mkoa, maarufu ‘bodaboda, Mohammed Iddy, amesema kujitokeza kupiga kura ni haki ya msingi ya kila mtanzania aliyefikisha umri wa miaka 18, na hatua hiyo inasaidia wananchi kupata viongozi wanaowataka wao wenyewe.
“Lakini ni muhimu kutunza amani yetu ili tuedelee kuwa huru kukusanya hizo Shilingi elfu moja moja kutoka kwenye biashara yetu.
“Kwa miaka mingi Tanzania inasifika kuwa nchi ya amani, hivyo tushirikiane kutunza tunu hii muhimu kwa kufuata utaratibu uliowekwa na mamlaka husika, ikiwemo kupiga kura na kuondoka,” ametoa wito
Katibu wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu wilaya ya Nyamagana, Shuwari Juma, ameunga mkono hoja, akawahimiza wananchi kurudi nyumbani baada ya kupiga kura, na kuacha suala zima la ulinzi wa kura mikononi mwa mamlaka zilizowekwa.
“Jeshi la polisi lipo pamoja na mawakala wa kila chama kitakachoshiriki uchaguzi, tuwaachie jukumu hili la kulinda kura,” ameshauri huku akisistiza wananchi kujitokeza kwa wingi kama katiba ya nchi inavyoelekeza kwamba kila baada ya miaka mitano ufanyike uchaguzi mkuu.
Msemaji wa Kongamano hilo ambaye pia ni mbunge mstaafu wa Jimbo la Nyamagana, Stansilaus Mabula, amesema kupiga kura ni moja ya kichocheo cha maendeleo katika jamii, baada ya wananchi kuchagua viongozi wanaowaamini katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.
“Na wakati huohuo tuzingatie umuhimu wa kutunza amani kwa kiwango cha juu,” amehimiza.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
My pay at least $300/day.My co-worker says me!I’m really amazed because you really help people to have ideas how to earn money. Thank you for your ideas and I hope that you’ll achieve more and receive more blessings. I admire your Website I hope you will notice me & I hope I can also win your paypal giveaway…….. https://cashprofit7.site