Mwenge kupitia miradi ya bil 65/- Kigoma

KIGOMA: Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake mkoani Kigoma ambapo utapita kwenye miradi 56  yenye thamani ya Sh bilioni 64.7. Ukiwa mkoani humo mwenge utatembea kilimotea 777.1 katika halmashauri nane za Kigoma.

Mkuu wa Mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro amesema hayo akipokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatuma Mwassa katika makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Nyakibuye Wilaya Kakonko mkoani Kigoma.

Balozi Sirro amesema kuwa katika miradi itakayopitiwa na mwenge miradi 16 itawekewa mawe ya msingi, mmoja utafunguliwa, 27 itazinduliwa na 12 itatembelewa.

Mkuu huyo wa mkoa amesema katika miradi inayotembelea na mwenge wananchi wamechangia Sh  milioni 283, halmashauri Sh bilioni 1.6, wahisani Sh bilioni 53 na Serikali Kuu ni Sh bilioni 6.6.

Katika siku ya kwanza ya mbio zake mkoani Kigoka Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa katika Wilaya ya Kakonko ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo, Evance Malasa amesema kuwa ukiwa wilayani humo mwenge huo wa uhuru utatembelea miradi saba yenye thamani ya Sh bilioni 2.2 ukikimbizwa kwa umbali wa kilometa 135.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button