Mwenyekiti CCM Wilaya ya Bariadi afariki dunia

MWENYEKITI wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Juliana Mahongo amefariki dunia leo Septemba 15, saa 1:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa, Lumen Ngunda imeeleza kuwa mwenyekiti huyo amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza.

Katika taarifa hiyo, Chama Cha mapinduzi Mkoa wa Simiyu, kimetoa pole kwa jamaa na marafiki kwa kumpoteza  na kiongozi wao.

Advertisement

CCM imemtaja Mahongo kama kiongozi ambaye alikuwa mtiifu, mwaminifu na mzalendo kwa chama chake.